Sunday, 29 September 2013

SAANAA NI ZAIDI YA UBUNIFU WASANII TUJITUME KUWEZA KUFIKIA MALENGO

Sanaa ya maigizo imekuwa ikikuwa kwa kasi siku za hivi karibuni hasa katika jiji la Dar es salaam.Tumeshudia vipaji vingi vikiibuka na wakongwe kuendelea kushikiria usukani wa gari hili.
Miaka ya 2000 tumeyaona majina makubwa Jacob Steven 'JB' ni mmoja wa mastar waliokimbiza sana miaka ya karibuni na kazi kama Lost Adam,My life zilizompa umaarufu mkubwa miongoni wapenzi wa Tasnia hiyo.Tumeshuhudia akiendelea kupiga bao na movie nyingine kama VITA BARIDI,NAKWENDA KWA MWANANGU  nyingine kama SHKAMOO MZEE inayoendeleea kutamba hadi kesho katika soko la filamu hapa bongo.
Wasanii wachanga tunaifunza nini kama somo kupitia kwa huyu mtu.Nimeongea na baadhi ya wasanii kutoka nyanda za juu kusini mikoa ya Iringa na Ruvuma na haya ndo maoni yao
Mwiba Namalove(Songea)

Wasanii tunahitaji kuwa na ushirikano baina yetu kama tunamalen

go ya kufikia walipo wenzetu.Sanaa si lelemama lazima tusimame,tukomae kweli kweli.Naamini tutafika kwani hata wao walitokea huku tulipo.
Lucksoni Dickson(Iringa)

 Kwa mtazamo wangu sanaa  inaweza kukua kwa msanii endapo atajua nini anahitaji kufanya.Wasanii wengi hatujitambui kwa kila kila kitu kuanzia fikra na hata mitazamo.Tunahitaji mabadiliko katika hilo.Mimi kama lucksoni napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wadau na mashabiki wa filam mkoani Iringa katika uzinduzi wa filamu yetu inayokwenda kwa jina la STRESS siku ya tarehe kumi na nane mwezi wa kumi katika ukumbi wa ISIMILA HOTEL hapa Iringa.


No comments:

Post a Comment