Sunday, 29 September 2013

CAMMY BOY-KIJANA ANAYEKIMBIZA KATIKA MUZIKI WA BONGO FLEVORS

Wengi wanamfahamu vizuri mkoani Ruvuma.Awapo stage huwa anajua nini kimemuweka,anajuanthamani ya mashabiki waliompokea na nini hasa watu wake wanahitaji.Nadiriki kumita the legend wa mkoa wa Songea.Wenyewe wanamwita Cammy G au Cammy boy.Katika maongezi yangu mafupi na Cammy anaiongeleaje sanaa ya mkoa wa Ruvuma?Haya ndo machache alioweza kunena nami
"Songea ni mji uliojaaliwa vipaji lakini ushirika,majungu na fitina imekuwa chachu ya kurudisha nyuma sanaa mkoa wa Ruvuma.Kimtazamo Wanasonge tunapaswa kua wamoja.Awe msanii wa sanaa ya maigizo,muziki au ngoma za asili tunapaswa kushirikiana.Inapaswa kwa msanii wa muziki  anapokutana na mwenzie wa maigizo amuone kama kaka,awe wa ngoma za asili basi ndugu yake.
Songea tunapaswa kujenga umoja unaoweza kututetea hata kesho tupatapo matatizo"
Cammy boy anapatikana mkoa wa Songea,msanii mwenye uchungu na sanaa ya mkoa wa Songea.Ifahamike Kwama Songea  inatoa majina kibao katika tasnia ya muziki na Tmathilia.
Ifamike kuwa Somgea ni moja ya sehemu zinazotoa vipaji.Majian kama Prof J,Roze Ndauka na Juma kilowako(marehemu mungu amrehemu huko Aliko.)yametokea mkoani hapo

SAANAA NI ZAIDI YA UBUNIFU WASANII TUJITUME KUWEZA KUFIKIA MALENGO

Sanaa ya maigizo imekuwa ikikuwa kwa kasi siku za hivi karibuni hasa katika jiji la Dar es salaam.Tumeshudia vipaji vingi vikiibuka na wakongwe kuendelea kushikiria usukani wa gari hili.
Miaka ya 2000 tumeyaona majina makubwa Jacob Steven 'JB' ni mmoja wa mastar waliokimbiza sana miaka ya karibuni na kazi kama Lost Adam,My life zilizompa umaarufu mkubwa miongoni wapenzi wa Tasnia hiyo.Tumeshuhudia akiendelea kupiga bao na movie nyingine kama VITA BARIDI,NAKWENDA KWA MWANANGU  nyingine kama SHKAMOO MZEE inayoendeleea kutamba hadi kesho katika soko la filamu hapa bongo.
Wasanii wachanga tunaifunza nini kama somo kupitia kwa huyu mtu.Nimeongea na baadhi ya wasanii kutoka nyanda za juu kusini mikoa ya Iringa na Ruvuma na haya ndo maoni yao
Mwiba Namalove(Songea)

Wasanii tunahitaji kuwa na ushirikano baina yetu kama tunamalen

go ya kufikia walipo wenzetu.Sanaa si lelemama lazima tusimame,tukomae kweli kweli.Naamini tutafika kwani hata wao walitokea huku tulipo.
Lucksoni Dickson(Iringa)

 Kwa mtazamo wangu sanaa  inaweza kukua kwa msanii endapo atajua nini anahitaji kufanya.Wasanii wengi hatujitambui kwa kila kila kitu kuanzia fikra na hata mitazamo.Tunahitaji mabadiliko katika hilo.Mimi kama lucksoni napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wadau na mashabiki wa filam mkoani Iringa katika uzinduzi wa filamu yetu inayokwenda kwa jina la STRESS siku ya tarehe kumi na nane mwezi wa kumi katika ukumbi wa ISIMILA HOTEL hapa Iringa.


TUJIKUMBUSHE KATIKA KAZI ZETU ZA NYUMA: ADELAHIDA

Kazi imefanyika  Songea -Ruvuma
Ni moja ya kazi zilizotamba katika tasnia ya filamu ikiwashirikisha wasanii wachanga wenye vipaji vya hali ya juu.
Hawa ni baadhi ya mastar wa kazi hiyo
Shukrani Faraji  Star wa Ahelahida Akiwa na mmoja wa washiriki kataika filamu hiyo iliyotoka mwaka jana.Kijana huyu yupo mbiani kuachia movie nyingine inayokwenda kwa jina la AFRICAN BIG MAMA kazi hiyo inayotarajiwa kuachiwa mapema mwezi ujao akimshirikisha nguli wa filamu hapa home MR JENGUA(MOHAMMEDI FUNGAFUNG)

Friday, 27 September 2013

HABARI NYEPESI:FILAMU YA STRESS KUZINDULIWA KWA KISHINDO-IRINGA

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu hatimaye kundi maana Mundu sanaa Group linatarajia kuzindua kazi yao mpya iendayo kwa jina STRESS.Filamu hiyo ikiwashirikisha mastar wakubwa wa Iringa kama Luckson Dickson Luswema ambaye ndo producer wa kazi hiyo na Athanas Kipera(Kibela).Pamoja Superstar kutoka Bongo movie Msanii Benny
HOLLOWW...........!
Filamu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa  mwezi ujao yaani October katika ukumbi utakaotangazwa hapo baadaye.Wapenzi na mashabiki wa filamu mkoa wa Iringa mnaombwa mkae mkao wa kula.Kwa mujibu wa Mr luckson itakuwa ni bonge la uzinduzi,haijawahi kutotea hapa The Stone Town(IRINGA)

NI NDANII YA BONGE LA UKUMBI   iSiMiLa HOTEL

18 october,wasanii  kibao wa kuimba na kuigiza watakuepo




MSANII WA WIKI

Katika maboresho ya blog yetu tumeanzisha ukurasa mpya utakaotumika kumtangaza msanii Chipukizi hivo basi wasnii mnaombwa kuwasliana nami katika matumizi ya ukurasa huu.
Msanii wetu leo ni Mwiba Namalove Ifuatayo ni profile yake kwa ufupi
JINA :Mwiba Namalove

KABILA:Mgoni


ALIKOZALIWA:Songea -Ruvuma


ANAKOISHI:Songea - Ruvuma




 

KUNDI ANALOIGIZIA:South Jemedari Arts




NAFASI  KATIKA SANAA:Katibu wa Songea Movie Club


Monday, 23 September 2013

KUMBE KUOA KUNA RAHA YAKE BWANA

Tarehe 21 mwezi huu ndani ya ukumbi wa St Domonic hapa Iringa tukio la Kihistoria lilifanyika tukimuaga Dada yetu kipenzi(SEND OFF PART)
Anaitwa  GRORY MDUDA ndiye tuliemuaga siku hiyo wakati akijiandaa kufunga pingu za maisha na Mr DAUDI MZIRAY pichani chini
Kama ndugu zake Gloria kwa pamoja tunamtakia kila la kheri ndugu yetu,dada yetu kipenzi katika safari yake ya maishayalilyo na changamoto za kila namna.Dada gloria tunafurahi kutuletea shemeji yetu,kwa hilo unastahili pongezi hasa ukizingatia jinsi dunia ilivyoharibika.
Mr Daudi kwa pamoja tunakukaribisha Iringa tuje kula Ka'mbwa pamoja ila tunaamini utakuwa mlinzi bora wa dada yetu.Kila la kheli katika hilo na MUNGU AWAPE MAISHA MAREFU yenye kheri na fanaka tele.
             BAADHI YA MATUKIO KATIKA SEND OFF HII

WE LOVE YOU ALL MR DAUDI MZIRAY & MISS GLORIA MDUDA


Saturday, 21 September 2013

MAONI YANGU:KARIBUNI IRINGA MTUPE UJUZI

Tunafurahi kutembelewa na wenzetu wa Tasnia ya uigizaji kutoka Dar es salaam hapa mkoani Iringa kifupi ni jambo jema  na la kujenga mahusiano bora baina ya wasanii.
 Tunapenda kuwashukuru kwa sababu zifuatazo
Moja tunajenga mahusiano ya kutambuana baina ya wasanii,kupima uwezo wetu  pia.
Pili kupata uzoef wa nini wenzetu mnafaya nasi kujaribu kutoka hatua tuliopo sasa kwenda nyingine angalau tupate kuwa katika level wenzetu mpo.
Pamoja na kuwashukuru kwa hilo basi tuombe uwaminifu katika hilo maana tayari Iringa tulisha umwa na nyoka kwa mfumo na utaratibu huo.
Ni kweli kabisa Sanaa tunaipenda lakini msitumie kigezo cha mapenz yetu ya Sanaa kuibia.Kwa pamoja tutajenga na kuiendeleza sanaaa

Thursday, 19 September 2013

Katika zoezi nzima la upigaji picha ya movie mpya msanii Khamis Nurdin Filam inaitwa 990 WAMEKUFA.Wasanii Kulwa kikumba(DUDE) pamoja Mohammed Fungafunga(JENGUA) wameshiriki pia katika kaz hiyo


Akiongea na Forever entertainment msanii Kulwa Kikumba(DUDE) akiwa Location ya kazi hiyo maeneo Mgama siku apiga picha za filamu hiyo akiwa na furaha anasema "Nimefurahi kufanya  kazi hapa mkoani Irnga napata exposure na kubadili mazingira yangu ya kazi,Tumekuwa tukifanyia kazi zetu Mkoan Dar es salaam lakini tunapopata nafasi kuja mikoan basi tunafurahi ki ukweli.
msanii huyu anasema anafurahia sana matunda yatokanayo na sanaa kwa sasa.

Mmoja wa mastar wa Africa Big Mama katika poz lake

Filam nyingine alizofanya ni pmoja na Adelahida(Vita dhidi ya mauaji ya Mapacha na Albino)
Anaitwa shukran Faraji wenyewe wanamuita mtoto wa Manispaa.Ndiye mmiliki na staring wa movie ya (African big mama)vita juu ya unyanyasaji wa wanawake.Akiongea na blog ya Forever entertainment Mr faraji amewaomba wakazi wa songea na maeneo ya jiran na songea na watanzania kwa ujumla kwamba watanzani wakae mkao wa kula kupokea bonge la filam ambayo imekutanisha vichwa vikubwa kwenye sanaa ya filam kama Mohammed Fungafunga(jengua).Either akaongeza kuwa yupo kwenye maandalizi ya filam nyingine ambayo hakuwa tayari kuitaja jina. 

Tuesday, 17 September 2013

BEHIND THE SCENE YA MY NUMBER ONE - DIAMOND

MTAZAME ALIYEFUNIKA FIESTA 2013 NDANI YA UWANJA WA JAMHURI MOROGORO.

MWANAFUNZI AMCHOMA KISU BABA YAKE MZAZI BAADA YA KUMWAMBIA AACHE MAPENZI NA ASOME...!!


DENTI wa Shule ya Sekondari ya Erkisongo iliyopo wilayani Monduli mkoani Arusha, anadaiwa kumchoma kisu katika paji la uso baba yake mzazi Daudi Msemo baada ya kuonywa kuachana na tabia ya kuchanganya ngono na masomo. Hayo yamesemwa na Fatuma Daudi ambaye ni mama mzazi wa mwanafunzi huyo mara baada kutokea tukio hilo la kusikitisha hivi karibuni nyumbani kwao Monduli ambapo denti alipofikishwa polisi alisema alifanya kitendo hicho kwa sababu baba yake alitaka kumbaka.“Binti yetu huyu amekuwa akibadilika tabia na mara nyingi tumekuwa tukimuonya aache vitendo vya umalaya akiwa mwanafunzi lakini bado amekuwa akiendeleza tabia...