Saturday, 6 September 2014

producer benny ashilikiana na khamis nurdin kuiua vipaji vya wasanii wa iringa kupitia studio george rec iliyopo wiloles wakiwa ndani ya miale sanaa group kama unajiona unakipaji wasaliana na benny kwa namba hii 0769 116165 au khamis nurdin 0715 698582




Wednesday, 23 April 2014

ETI HAWA WAREMBO WANADAI WASHAWAHI...........NA ALI K

Ali kiba ni mmoja wa wanamuziki walio kimya sana kwenye upande wa kuongelea mambo yake binafsi, haswa kimahusiano, au hata kujitangaza kumiliki kitu kingine chochote cha thamani kama ilivyo desturi ya wasanii wengi hapa town baada tu ya kupata umaarufu, ila siri hufichuka haswa pale kwa warembo hawa wanapoamua kumwaga mpunga ndipo hapo unapoanza kujua yaliyo chini ya kapeti.Hawa ni warembo waliowahi kukiri kuwa walishawahi kuwa na mahusiano na Celeb huyu mkongwe sana kwenye anga za muziki huu wa Bongo Fleva.
 collagbhveMapenzi ya hawa wawili inasemekana yalianza enzi hizo ambapo wawili hao walikuwa bado hawana majina kabisa hapa town, kila mmoja wao akiwa yupo kwenye hustle zakutoka kila mmoja akiwa natetea fani yake, ila kwa bahati nzuri AliKiba akaanza kupata umaarufu kuitia muziki hata kabla ya Wolper kuanza ku-make headlines kupitia filamu, akiwa kama muigizaji.

“Ni kitambo kidogo sana wote hatukuwa star lakini mwenzangu alifanikiwa kuchomoka,lakini Ali ndiye aliyeniingiza kwenye ulimwengu wa Mapenzi” alifunguka Wolper,
“Ali akawa star,alipokwenda nje nikasikia wanawake wanamshobokea,sasa mimi sikutaka karaha nikakaa pembeni,lakini jamaa ni mtu poa sana na tukikutana tuanasalimiana freshi kabisa” alimalizia akizungumzia sababu zilizomfanya aachane na Kiba wakati huo.

Lulu Michael.
cohllage
haikujulikana mapema kama inavyotokea kwa watu maarufu wengi hapa town, ila mahusiano yao yalianza huko kitabo sana, baina ya Lulu na Ali Kiba, ila mwisho wa siku Lulu aliamua kumwaga mpunga hadharani kufunguka juu ya mahusiano yao.

“Duh! Umenikumbusha mbali sana. Nilishasahau kabisa kama niliwahi kutoka naye. Pamoja na kwamba ni kweli alikuwa mtu wangu, lakini kwa sasa moyo wangu hautaki kusikia kingine zaidi ya Bieber na namuonea wivu sana Selena Gomez (mpenzi wa Bieber).”

ila hakutaka kuzungumzia sababu za kuachana naye, nakusea ilikuwa tu sababu zake binafsi kwa sababu mapenzi yana taba moja kuwa ukiyag’ngania hasa pale ambapo hauenjoy mwisho wake ni kuumizana tu, alimalizia lulu kuelezea safari yake ya mapenzi, na hadi hivi sasa anakiri kuwa bado yupo

Wednesday, 16 April 2014

MAONI YA SHEKH SHARRIF HAMAD KUHUSU MUUNGANO MH....!


  Hammad ambaye kwa siku za karibun amekuwa mmiliki wa vichwa vya habari kutokana na ripoti mbalimbali ambazo zimekua zikimnukuu kwa kudai kutozitaka serikali mbili lakini leo April 15 2014 amezungumza kwenye maonyesho ya miaka 50 ya muungano ya kuzitoa hizi kauli zifuatazo.
1. ‘Pamoja na milima na mabonde, muungano huu umedumu miaka 50, nchi nyingine zilishindwa, lazima tufanye tathmini hasa ya muungano wetu, lazima vijana waelimishwe vp muungano uliundwa, tulianzia vipi’
2.‘Ukitaka upate maenedeleo, yatambue mafanikio yako lakini pia usisahau matatizo yako, ni ni moja.. kufanya vizuri, Sidhani katika Tanzania kama kuna watu hawataki muungano, na kama wapo ni wachache, muungano uendelee ndio la msingi’
3. ‘Sio dhambi watu kuwa na fikra tofauti, sio dhambi hata kidogo kwa sababu hatuwezi wote kuwa na fikra aina moja, Wanaotaka serikali moja wasibezwe, mbili wasibezwe, wanaotaka tatu na serikali ya mkataba wasikilizwe pia’
4. ‘Wako wanaoamini kwamba matatizo ya muungano yako kwenye muundo, tuwasikilize wana hoja gani, Mwaka 1963 Malaysia na Tanganyika maendeleo ya sehemu zote hizi yalikua sawa, mwaka 2014 tujiulize, changamoto kwetu ni vipi tutakua na muungano utakaokua ni chachu ya maendeleo ya haraka, mambo ya 74 ni tofauti na 2014′
5. ‘Tuwe makini sana, sote ni wa nchi moja, tujiepushe na kikundi chochote kuona wao wana haki zaidi, Watanzania wote sawa, wajumbe wa bunge maalum waangalie maslahi ya nchi, muungano huu ni wa nchi 2 zilizokua dola huru na kuungana kwa hiari’
6. ‘Tupate katiba ambayo itaondoa migogoro, kero iwe ni historia… hili swala lisiwepo tena, tusiende kwenye maamuzi ya harahaharaka tukasema serikali mbili au tatu bila kuangalia athari zake, katiba ya Znz inasema ni miongoni mwa nchi mbili za muungano, ya Muungano inasema Tz ni nchi moja, huo ni mgogoro’
7. ‘Nadhani Warioba walivyopendekezwa waliona hisia za Znz zilivyo, tunataka katiba itakayotambua usawa wa nchi mbili, hakuwezi kuwa na katiba ambayo itamridhisha kila mtu lakini angalau wengi wao waridhike’

Mbunge wa Mbeya mjini amwaga cheche bungeni jana

"Mwigulu Nchemba anataka Serikali moja, lakini anaogopa kusema"........... "Mhe.Mwenyekiti, kwanza naunga mkono Serikali tatu kama zilivyoletwa kwetu na TUME ya Katiba ya Jaji Warioba, kwa hiyo tunaunga mkono maoni Wananchi. Aliyeuharibu huu mchakato ni RAIS aliyekuja kueleza msimamo wa Chama chake badala ya kuzindua Bunge. Hiki ni Kipindi cha Kwaresma, acheni unafiki, tumeharibu Pesa nyingi. CCM wameishiwa hoja, wameanzisha mkakati wa kuzomea. MWIGU...LU anataka Serikali moja, lakini anaogopa kusema. Tupo kwenye nafasi nzuri sana ya kulijadili Swala hili, la sivyo, tutalijadili kwa kulazimishwa. Leo LUKUVI anatutishia uwepo wa Serikali tatu, JESHI litaitawala Nchi! Mbona Rais wetu alikuwa Mwanajeshi na anatuongoza?...Wanajeshi ni Ndugu zetu, wakitawala kuna tatizo gani?... Unapopimwa Malaria au Ukimwi, Sample ya Damu inatolewa kidoleni, na sio lita tano ili kujua ngoma imekaaje mwilini! acheni kutuzingua kwamba waliohojiwa na TUME ya Warioba ni wachache". amesema Mhe.Sugu.

Thursday, 10 April 2014

Tuesday, 8 April 2014

WE..MWANAUME FANYA HAYA KAMA UNATAKA KUEPUKA KUCHUNWA NA MADEMU

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhis4Liy1yfJkaw0imNQwOzzs_QontxC-ZL4WZ4uXKQF_kmrymLpTQT703h10rVFtwxjE-2HOn4nDKpiRBpu6vEUTfvf8t3eit5bH_9znU_tYSm51I0Xy-dDEMy80LLWofEa6373ddFBwM/s1600/aa-couple-laying-in-bed.jpgNaongea na wale ambao tayari wamesha jitegemea kimaisha, ambao hawaishi na wazazi wao, wanaokumbana na mkono wa Mama/Baba mwenye nyumba kila baada ya miezi sita mitatu au mwaka..
Wanaoishi ki-bachelor lakini wana wapenzi.
Katika hii movie ya ki-bachelor tunakumbana na mengi sana,,kuna wanaogeuza ma girl friend zao kuwafanya kama mke,,tabia ya aina hii imepelekea na wao kugeuzwa kama waume,,hapa unakuta kila kitu girlfriend anakutegemea wewe akipata kashida kidogo ooohh baby nataka hela..

Mazingira ya kuchunwa tunayatengeneza wenyewe usianze kumhisi binti wawatu ni mchwa,,jichunguze kwanza na wewe kinachofanya akunyoshee mkono.
Ukiweza kuyamudu mambo yaha hakika hautayachukia maisha ya ki-bachelor na kumgeuza girl friend kuwa mke, na yeye pia atashindwa kupata ujasiri wa kukutegemea kiasi fulani labda tu kama nitabia yake..

1. Kujipikia
2. Kufua
3. Usafi wa vyombo.
4. Usafi wa chumba.


Ukiweza kukabiliana na hayo pasipo kutegemea msaada kutoka kwa girl wako utayafurahia sana maisha ya ki-bachelor,,na swala la kuoa kwako utaliamua kwa wakati muafaka, ila sio kwa kuwa unahitaji msaidizi.

Ebu fikiria labda girlfriend wako anakuja kukusalimia siku ya mapumziko, anakuta chumba chako umesafisha vizuri vyombo viko katika mpangilio mzuri,,umefua nguo zako na mashuka,,huku na huku haujachoka kuna akiba ya mchele,,unawasha kajiko kako unapikia wali na unaandaa mboga yani kila kitu unaweka sawa kisha unapakua kwenye hotpot yako, basi akija mnakula kama atapenda,,baada ya chakula mnaendelea na mambo yenu,,kusanya vyombo vyako akiondoka unaviosha.

Kumbuka kufanya hivyo hakuondoi uan
aume wako,,jifunze kudhamini vitu vyako girlfriend hajawahi kukununua hata kijiko vyote umenunua kwa pesa yako,,ulio itolea jasho kwa kugombania daladala asubuhi uwahi kazini.

Hapo unajaribu kutengeneza mazingira ya kumfanya asijihisi unamtegemea sana zaidi ya kitu kimoja tu nadhani unakijua kwa wale mabachelor ambao mnamiliki kiwanja cha fundi selemara chumbani kwako.

Kama bachelor mwenye akili zako timamu lazima uishi kwa malengo ukijua kesho na wewe utakuwa na familia itaishi vipi kama ukiendekeza kuhonga katika ubachelor wako.

Ishi na mwanamke kwa kanuni kama unavyo fanya hesabu,,baada ya hayo kinachofuatia hakikisha unatumia kiasi kidogo sana cha pesa kumnunulia vitu vidogo vidogo ambavyo havina gharama,,ili mkusahaulisha kiasi fulani auone uwepo wako.

Ila kama wewe sio muoga kama mimi basi unamkazia kabisa,,maana demu nae akishajua unapenda pochi manyoya yake basi atakubabaishia,,,usiwe mtumwa wa pochi manyoya.

Kwa style hiyo binti unasababu ya kumtegemea boy wako???

Na wewe bachelor mwenzangu hapo bado unayo sababu ya kugeuzwa kitega

uchumi?????

Friday, 4 April 2014

Only one day left.Dont MISS IT

BASI LA PRINCE MURO LAUA MTEMBEA KWA MIGUU IRINGA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjVombuwg2t4mudAhYumYEE4qTl5qjXPjOazlBJGGZBFG5PGUM9Uhtbb3UO1hcncpIBtGj7qO_jx5hLydKflMVQugn_7j25_OYICxznOvv2S2VZnL3bpL3SVdSkU8QZP-b3Gfsv9lVD0VxQ/s1600/rpc.jpg
JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia dereva wa basi la abiria la Prince Muro, ambalo hufanya safari zake kati ya Mbeya na Dar es salaa, Said Mtatifikolo, kwa tuhuma za kumuua mtembea kwa miguu baada ya kumgonga.
Kaimu Kamanda wa jeshi hilo, Nyingesa alisema kuwa ajali hiyo, imetokea juzi jioni katika eneo la Viwengi wilayani Iringa.
Nyigesa alisema ajali hiyo ilitokea baada ya basi hilo lenye namba za usajili T 528 BVP, kumgonga na kumuua mtembea kwa miguu ambaye jina lake bado halijafahamika kutokana na mwili wake kuharibika.
Hata hivyo alidai kuwa upelelezi juu ya ajali hiyo unaendelea na kwamba, mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika.
Katik tukio jingine, Mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Mgama, wilayani Iringa Jesca Chaula(9), amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye dimbwi la maji.
Kaim Kamanda, Nyigesa alisema tukio hilo limetokea jana kijijini hapo ambapo, mwanafunzi huyo akitokea shule alitumbukia kwenye dimbwi lamaji na kufa kwa kukosa msaada wa haraka.
Aliwataka wananchi, kufukia madimbwi ya maji kwenye mazingira yao ili kuokoa maisha ya watoto ambao wamekuwa wakipotea kwa kutumbukia.
Mwisho.

download nyimbo mpya Prof J v/s Diamond here

http://www.hulkshare.com/hassbaby/professor-jay-ft-diamond-kipi-sijasikia

Tar 6/4 Zimanimoto Songea kuwaka Moto

Photo

UNAMJUA WAJE?STAR WA NIGERIA ALIYESHIRIKISHWA NA DIAMOND PLATNUMZZZ KATIKA NYIMBO YAKE MPYA?

Ndo huyu,kweli dogo anakismet.

Thursday, 3 April 2014

VIDEO MPYA YA SHILOLE MAJAANGA!

Kwa video hii SHILOLE kaazi kweli!

MAN OF THE DAY

Ni msomi wa chuo kiku cha mtakatifu Joseph tawi la Songea katika fani ya Sayansi ya Computer na ualimu.
JINA:SIMON NGANYANYUKA
UMRI:private
KAZI:MWALIMU AND COMPUTER PROGRAMMER
ANACHOPENDA:MPIRA,MUSIC AND STUDYING AND CHARTING WITH FRIENDS
INTERESTED:LADIES
Follow nhim on facebook for communication

Monday, 24 March 2014

COLONEL MUSTAPHA ALIA NA MAANDAMANO YA UDHALILISHAJI WA MWANAMKE KUFUATIA KUTUPIA PICHA CHAFU AKIWA NA HUDDAH....

http://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/03/Screen-Shot-2014-03-25-at-1.29.26-AM.png
Colonel Mustapha ni miongoni mwa Wasanii wa longtime kidogo kwenye game ya muziki Kenya toka enzi hizo akiwa kwenye kundi lililotoa hit single yenye maneno ‘bibi yake mufupi, kijana murefu ametoka wapi’
Hivi karibuni ameingia kwenye vichwa vya habari sana hasa baada ya kutangaza kuwa mapenzini na Huddah, mrembo aliewahi kuiwakilisha Kenya kwenye shindano la Big brother Africa ambapo uhusiano wao hauchukua muda mrefu ukavunjika.
Kabla ya kuvunjika, tayari walikua wameshapiga picha ambapo Mustapha anasema alikua amerekodi wimbo na Huddah lakini walipoachana mrembo huyu akasema Ogopa Dj’s wasiitumie tena sauti yake kwenye huo wimbo na kama watafanya hivyo atawashitaki.
Hata hivyo picha zao wawili zilishasambaa kwenye internet tayari na kuanza kuchukua headlines kutokana na pozi zao.
http://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/03/Screen-Shot-2014-03-25-at-1.29.51-AM.png?resize=469%2C609Kuonyesha kupinga hiki kitendo, mwimbaji staa wa ‘watu na viatu’ Nyota ndogo aliungana na Wanawake wengine Mombasa na kuandamana kupinga kitendo cha Mustapha kuzisambaza picha zinazomdhalilisha Mwanamke hivyo aombe msamaha haraka iwezekanavyo.http://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/03/Screen-Shot-2014-03-25-at-1.30.18-AM.png
akisema ‘Mustapha ambae ni msanii mkubwa ameanza muziki kitambo kuchukua picha za watoto wa kike na kuwavua nguo, hii itanyima hata Wazazi kuachia watoto wao kufanya muziki unaoonekana uhuni… ikiwa Mustapha hatoacha hii itatuharibia, kama kaona ameshindwa kutunga nyimbo zitazowashika watoto wa sasa hivi afate mtoto amuandikie’
‘Ameona jina linashuka ndio maana bora achukue picha za uchi atengeneze skendo, Mustapha nimekua nae kwenye muziki miaka mingi, kwa nini sasa hivi ndio afanye kwa sababu Prezzo anafanya? ama ameona Prezzo yuko juu kwa sababu anafanya.. yeye ndio anatakiwa kumwambia Prezzo usifanye hivi’
 
Screen Shot 2014-03-25 at 1.34.45 AMScreen Shot 2014-03-25 at 1.35.12 AM
Hata hivyo Mustapha amezungumza baada ya haya maandamano na kusema ‘Ni kitu cha kushtua kuona maandamano yamefanyika kwa ajili ya Mustapha, wakati tunapiga hizi picha hakukua na lengo lolote la kumdhalilisha Mwanamke bali ilikua mambo yetu yenyewe kwa raha zetu, nilivyoona youtube kuhusu haya maandamano nimehuzunika… naomba msamaha kwa yeyote aliekerwa na hili… nimekubali kuomba msamaha kwa Wanawake’
Kwa kumalizia Mustapha amesema ‘kuna Wasichana ambao wanataka tupige hizo picha na wananilipa’
Screen Shot 2014-03-25 at 1.37.19 AM

Sunday, 23 March 2014

KWA NINI MASHOGA WANAONGEZEKA BONGO?

Nimepita pita huko mitaani hasa Kinondoni, kwenye mahotel ,ma bar na kumbi za starehe, Nimeshangaa sana kuona wakaka poa kibao, tena wamejiremba kama wadada vile, nao wakijiuza kama machangudoa, nini hasa tatizo ?? 

embu toeni comment zenu hapa na mwono wako juu ya swala hili labda tunaweza pata wazo jipya kuhusiana na hili maana hali inazidi kila kukicha
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhCF6AooHmjgH44GIi7ek7I_lphRyHhDH12VXDppGuKzze4hF1d1xEgS-6cssU0hof43wDnHW7BOg-FqnI85pZTnskpvqyvJWbOmRx5gNCHwgPnc0Avsk_WgS3hdiaKWsky1ZdqYNjWi-U/s1600/shog.jpg

Thursday, 13 March 2014

Salamu kwa wanablog wa forever entertainment

Bila shaka ni wazima wasomaji wetu ni wazima .Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi wafuatiliaji wa blog hii kwa kutokuwapo hewani kwa muda mrefu kutokana na matatizo yalio nje ya uwezo wetu.Kwa pamoja kama ofisi tunawaahidi kuwa tumerud rasmi katika kazi.Twende kazi ufurahi nasi

Tuesday, 4 February 2014


tazama picha za uwanja mpya uliyoppo mjini iringa na hivi karibuni kundi la miale sanaa group lilienda kucheza mechi pamoja na waandishi wa habari wa redio nuru ambapo miale sanaa group iliondoka kwa ushindi wa magori 14 kwa 5 zidi ya wapinzani wao waandishi wa habari wa redio nuru

 huyu ni khamis nurdin mkurugenzi wa kundi la miale sanaa group akiwa wanjani

 awa ni mashabiki pamoja na wachezaji wa miale sanaa group

 hawa ni miale sanaa group wakiwa ndio wanaingia wanjani kwajili ya mechi na waandishi wa habari wa redio nuru

 waandishi wa habari wa redio nuru wakiwa ndio wanaingia wanjani kwajili ya mechi na miale sanaa group

 wasanii wa miale sanaa group wakiwa wanautizama mpila kwa umakini sana huku wakisubiri sabu

 timu zote mbili zikiwa wanjani zikicheza mechi ni miale sanaa group na waandishi wa habari wa redio nuru