Wednesday, 16 April 2014
Mbunge wa Mbeya mjini amwaga cheche bungeni jana
"Mwigulu Nchemba anataka Serikali moja, lakini anaogopa
kusema"........... "Mhe.Mwenyekiti, kwanza naunga mkono Serikali tatu
kama zilivyoletwa kwetu na TUME ya Katiba ya Jaji Warioba, kwa hiyo
tunaunga mkono maoni Wananchi. Aliyeuharibu huu mchakato ni RAIS
aliyekuja kueleza msimamo wa Chama chake badala ya kuzindua Bunge. Hiki
ni Kipindi cha Kwaresma, acheni unafiki, tumeharibu Pesa nyingi. CCM
wameishiwa hoja, wameanzisha mkakati wa kuzomea. MWIGU...LU
anataka Serikali moja, lakini anaogopa kusema. Tupo kwenye nafasi nzuri
sana ya kulijadili Swala hili, la sivyo, tutalijadili kwa kulazimishwa.
Leo LUKUVI anatutishia uwepo wa Serikali tatu, JESHI litaitawala Nchi!
Mbona Rais wetu alikuwa Mwanajeshi na anatuongoza?...Wanajeshi ni Ndugu
zetu, wakitawala kuna tatizo gani?... Unapopimwa Malaria au Ukimwi,
Sample ya Damu inatolewa kidoleni, na sio lita tano ili kujua ngoma
imekaaje mwilini! acheni kutuzingua kwamba waliohojiwa na TUME ya
Warioba ni wachache". amesema Mhe.Sugu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment