Naongea
na wale ambao tayari wamesha jitegemea kimaisha, ambao hawaishi na
wazazi wao, wanaokumbana na mkono wa Mama/Baba mwenye nyumba kila baada
ya miezi sita mitatu au mwaka..
Wanaoishi ki-bachelor lakini wana wapenzi.
Katika
hii movie ya ki-bachelor tunakumbana na mengi sana,,kuna wanaogeuza ma
girl friend zao kuwafanya kama mke,,tabia ya aina hii imepelekea na wao
kugeuzwa kama waume,,hapa unakuta kila kitu girlfriend anakutegemea wewe
akipata kashida kidogo ooohh baby nataka hela..
Mazingira
ya kuchunwa tunayatengeneza wenyewe usianze kumhisi binti wawatu ni
mchwa,,jichunguze kwanza na wewe kinachofanya akunyoshee mkono.
Ukiweza
kuyamudu mambo yaha hakika hautayachukia maisha ya ki-bachelor na
kumgeuza girl friend kuwa mke, na yeye pia atashindwa kupata ujasiri wa
kukutegemea kiasi fulani labda tu kama nitabia yake..
1. Kujipikia
2. Kufua
3. Usafi wa vyombo.
4. Usafi wa chumba.
Ukiweza
kukabiliana na hayo pasipo kutegemea msaada kutoka kwa girl wako
utayafurahia sana maisha ya ki-bachelor,,na swala la kuoa kwako
utaliamua kwa wakati muafaka, ila sio kwa kuwa unahitaji msaidizi.
Ebu
fikiria labda girlfriend wako anakuja kukusalimia siku ya mapumziko,
anakuta chumba chako umesafisha vizuri vyombo viko katika mpangilio
mzuri,,umefua nguo zako na mashuka,,huku na huku haujachoka kuna akiba
ya mchele,,unawasha kajiko kako unapikia wali na unaandaa mboga yani
kila kitu unaweka sawa kisha unapakua kwenye hotpot yako, basi akija
mnakula kama atapenda,,baada ya chakula mnaendelea na mambo
yenu,,kusanya vyombo vyako akiondoka unaviosha.
Kumbuka kufanya hivyo hakuondoi uanaume
wako,,jifunze kudhamini vitu vyako girlfriend hajawahi kukununua hata
kijiko vyote umenunua kwa pesa yako,,ulio itolea jasho kwa kugombania
daladala asubuhi uwahi kazini.
Hapo
unajaribu kutengeneza mazingira ya kumfanya asijihisi unamtegemea sana
zaidi ya kitu kimoja tu nadhani unakijua kwa wale mabachelor ambao
mnamiliki kiwanja cha fundi selemara chumbani kwako.
Kama
bachelor mwenye akili zako timamu lazima uishi kwa malengo ukijua kesho
na wewe utakuwa na familia itaishi vipi kama ukiendekeza kuhonga katika
ubachelor wako.
Ishi
na mwanamke kwa kanuni kama unavyo fanya hesabu,,baada ya hayo
kinachofuatia hakikisha unatumia kiasi kidogo sana cha pesa kumnunulia
vitu vidogo vidogo ambavyo havina gharama,,ili mkusahaulisha kiasi
fulani auone uwepo wako.
Ila
kama wewe sio muoga kama mimi basi unamkazia kabisa,,maana demu nae
akishajua unapenda pochi manyoya yake basi atakubabaishia,,,usiwe mtumwa
wa pochi manyoya.
Kwa style hiyo binti unasababu ya kumtegemea boy wako???
Na wewe bachelor mwenzangu hapo bado unayo sababu ya kugeuzwa kitega
uchumi?????
No comments:
Post a Comment